Jumamosi 23 Agosti 2025 - 11:13
Mufti wa Jaafari Lebanon: Iran ni chimbuko la heshima ya kila mwanadamu huru katika ulimwengu huu na uaminifu wetu kwa Tehran ni kama uaminifu wetu kwa Mawalii wakuu

Hawzah/ Sheikh Ahmad Qabalan amesema: Iran ndiyo iliyouangamiza mradi wa Mashariki ya Kati na ikaibatilisha matumaini ya Washington na Tel Aviv yanayotokana na ugaidi, uvamizi pamoja na uharibifu

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, mwanazuoni wa Kishia na Mufti mashuhuri wa Jaafari, katika tamko lake amesema: Kwanza namwambia Bashara Butrus al-Ra‘i (Askofu wa Wamaroniti Wakristo wa Lebanon): Amani, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako, kwani amani ni hazina ya manabii, na kwa kuwa kumpinga dhalimu ni dini ya Mawalii, na kwa kuwa nguzo ya Kanisa na Msikiti haiwezi kusimama ila kwa kusimama pamoja na wanyonge, kuwasaidia masikini, kuwafariji wenye mateso na kukabiliana na madhalimu, waovu, wanyanyasaji na madhalimu kama Israeli, mshirika wake, mradi wake wa kigaidi na historia yake iliyozama katika mateso ya Masih na Wakristo.

Silaha ya Hizbullah na Harakati ya Amal ni silaha ya Mwenyezi Mungu

Akaongeza kwa kusema: Silaha ya Hizbullah na Harakati ya Amal ni silaha ya Mwenyezi Mungu, na hakuna nguvu yoyote duniani itakayoweza (kwa idhini ya Mwenyezi Mungu) kuizima, na nafsi zetu, uhai wetu na uwezo wetu wote, ulio tayari kulitetea taifa hili la Lebanon vipo pamoja na harakati hiyo. Sisi ni nguvu ambayo Mwenyezi Mungu ameibariki kwa kujitolea kihistoria na ushindi wa kitaifa, licha ya kupigwa watu waliokuwa karibu nasi.

Mwanazuoni huyo wa Kishia wa Lebanon amebainisha kuwa: Ikiwa Lebanon ya kisasa ina fidia na kafara ya kihistoria, basi ni ile iliyotolewa na Harakati ya Amal, Hizbullah na vikosi vyote vingine vya Muqawama, ambavyo viliishinda Israeli na kuiodosha nguvu yake kutoka katika serikali ya Lebanon, taasisi zake na sekta zake mbali mbali, kuficha ukweli si jambo linalowezekana ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kulipiza kisasi kiholela si mantiki ya Kanisa wala ya Msikiti.

Uamuzi wa kuwanyang'anya silaha Muqawama ni uamuzi wa kijinga, batili na usio na thamani

Sheikh Qabalan alisema: Makubaliano thabiti ya kikundi kidogo cha watu wasio na uhusiano wowote na uzalendo, ya kutekeleza uamuzi wa kuchukua silaha za Muqawama, ni uamuzi wa kijinga, batili na usio na thamani, na thamani yake ni sawa na thamani ya wino ulioharibika ulioandikiwa, hakuna uamuzi wa khiyana zaidi kwa nchi hii, historia na mamlaka yake, kuliko uamuzi huu, uamuzi huu ni wa manufaa makubwa zaidi kwa utawala wa Kizayuni na una uzito wa kitaifa wa sifuri, hatutawaruhusu Wazayuni kuikalia tena Lebanon (in shaa Allah).

Mufti mashuhuri wa Jaafari akaendelea kwa kusema: Mategemeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu, kwa watu hawa wapenzi, kwa jeshi lao la kitaifa na kwa Muqawama wao mkubwa unaosubiri nyakati za kujitolea kubwa, wana wa Kishia wamechoshwa na kujisalimisha, khiyana na shahada za uongo, ikiwa kuna taifa moja katika nchi hii lililo tayari kujitolea damu yake, vijana wake na nguvu zake kubwa kwa ajili ya taifa hili tukufu, basi ni taifa la Kishia, yaani taifa la Muqawama kwa sura na nyanja zake zote.

Akaashiria kwamba: Maneno ya ndugu yetu mpenzi, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qasim, yamejaa ukweli na misimamo wa kizalendo, yeye maisha yake yote ameyatumia kuuhisha Lebanon na kuhifadhi mamlaka yake, na ataendelea kufanya hivyo.

Sheikh Qabalan akaongeza kwa kusema: Kabla yake na baada yake, maneno ya kuaminiwa na taifa na nchi, mnyanyua bendera wa kujitolea kitaifa na mbebaji wa amana ya Imam Musa Sadr, ndugu yetu mpenzi, Spika Nabih Berri, ambaye katika harakati ya Februari 6 alilinyakua tena taifa na baada ya taifa kupotea na baadhi kushirikiana na Uzayuni, aliingia katika uwanja wa Muqawama mkubwa, bado yanavuma, Nabih Berri bado ni ngao ya Lebanon na mwenye busara wa mamlaka yake ya kitaifa.

Akaendelea kusema: Hizbullah ni Harakati ya Amal, na Harakati ya Amal na Hizbullah zinamaanisha Ushia, na Ushia maana yake ni kila mtu huru katika nchi hii tukufu kwa Muqawama wake, kujitolea na uzalendo wake, Hizbullah haijawahi kupenywa wala haitapenywa, na haijashindwa wala haitashindwa, ndio iliyolishinda jeshi lenye nguvu zaidi la NATO la Israeli katika mpaka pamoja na ghala lake kubwa la silaha na msaada kamili wa washirika wote wa Israeli.

Sheikh Qabalan akaendelea kusema: Hizbullah ndiyo iliyotoa ulinzi hatari zaidi wa kitaifa mbele ya ghala kubwa la silaha la Israeli-Atlantiki na kwa uwezo wake wote ilizuia uvamizi wa miji ya mpakani kama Khiam na nguvu hizo kubwa, na iliangusha mradi wa Mashariki ya Kati kupitia bahari ya damu, maiti na kujitolea, tuna matumaini kwamba Kanisa litaendelea kuwa Kanisa, Msikiti kuwa Msikiti, na serikali ya Lebanon kuwa serikali huru na haramu kwa Uzayuni na miradi ya Mei 17.

Iran ni chimbuko la heshima ya kila mwanadamu huru duniani

Akaashiria kwa kusema: Iran ni chimbuko la heshima ya kila mwanadamu huru katika ulimwengu huu, uaminifu wetu kwa Tehran ni kama uaminifu wetu kwa Mawalii wakuu, Mawalii wa Mwenyezi Mungu hawana adui isipokuwa mashetani, kwa ukumbusho, nasema: Iran ndiye aliyeuangamiza mradi wa Mashariki ya Kati na akabatilisha matumaini ya Washington na Tel Aviv yanayokua kwa ugaidi, uvamizi na uharibifu.

Mwanazuoni huyo wa Kishia wa Lebanon alisema: Iran ndiye aliyeziweka mbali Washington na Tel Aviv na ndoto ya Israeli Kubwa, kauli mbiu ya Muqawama kwa nusu karne haijawahi kudondoka, na haitadondoka maadamu nchi inahitaji ulinzi, hifadhi na kujitolea, hatujashindwa vita, na (in shaa Allah) hatutashindwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha